Mussa Bakari (21) a Ibrahim Shabani (28), wote wakazi wa Kijiji cha Mkangaula, Kata ya Namalenga wilayani Masasi mkoani Mtwara, wameuana baada ya kupigana kwa kutumia magongo wakigombea mwanamke aliyetambulika kwa jina la Hadija Msamati, kila mmoja akidai ni mpenzi wake.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicomedus Katembo, alisema lilitokea mwishoni mwa wiki majira ya saa 12 jioni katika Kijuji cha Mkangaula wilayani Masasi mkoani hapo.
Kamanda Katembo alisema vijana hao waliuana baada ya kugombea mwanamke ambaye kila mmoja alidai ni mpenzi wake, hivyo walipofumaniana walianzisha ugomvi na kupigana kwa kutumia magongo.
Alisema kuwa baada ya ugomvi wao, wote wawili walipigana na kusababisha kuuana, vifo vyao vikisababisha taharuki kwa jamii kwa kuwa tukio hilo siyo la kawaida katika maeneo hayo.